Kiswahili
Tunaalika shirika lako litume mapendekezo (watakaozingatiwa) kwa Tuzo la 2025 (la 22 linalokuwepo kila mwaka) linaloitwa Stevie® Awards for Women in Business (Tuzo la Stevie® Awards la Wanawake walioko kwenye Biashara). Mpango wa kwanza kabisa wa matuzo ya biashara katika ulimwengu mzima hasa kwa wanawake umetayarishwa na waundaji wa matuzo ya prestigious International Business Awards® na American Business Awards®.
Ikiwa ungependa kupokea fomu/kifurushi cha kuingilia, chenye maagizo kamili kuhusu jinsi ya kutayarisha na kutuma mapendekezo yako (watakaozingatiwa kwa tuzo hili), tuma barua pepe yako hapa na tutakutumia kifurushi hicho au fomu hiyo. Tuko na sera mathubuti sana ya faragha na hatutashiriki (kuambiana) barua pepe yako na wengine, kwa sababu yoyote ile.
Huu ndio ukurasa pekee kwenye tovuti hii ambao utaona ukiwa umeandikwa kwa lugha hii. Kurasa nyingine zote na hata fomu ya kuingilia zimeandikwa kwa Kiingereza. Zimeandikwa kwa Kiingereza kwa sababu tunahitaji kwamba mapendekezo (watakaozingatiwa kwa tuzo) yatumwe kwa lugha ya Kiingereza, ili wataalamu wa biashara ulimwenguni kote waweze kushiriki kwenye mchakato wa kutoa maoni na kuamua. Ifuatayo ni muhtasari kuhusu tuzo la Stevie Awards for Women in Business (Tuzo la Stevie Awards la Wanawake walioko kwenye Biashara), yanayohitajika unapotuma au kuwasilisha mapendekezo yako na manufaa ya kushiriki. Ukiamua kwamba shirika lako litatuma mapendekezo (watakaozingatiwa kwa tuzo) la Stevie Awards for Women in Business (Tuzo la Stevie Awards la Wanawake walioko kwenye Biashara), kumbuka kwamba mapendekezo yako lazima yatayarishwe kwa lugha ya Kiingereza.
Tuzo la Stevie Awards for Women in Business (Tuzo la Stevie Awards la Wanawake walioko kwenye Biashara) hutuza mafanikio ya wanawake wafanya biashara, wajasiriamali, wakurugenzi, waajiriwa na mashirika ambayo wanaongoza, ulimwenguni kote. Shirika la Stevie Awards, linalopatiana matuzo haya, lipo nchini Marekani. Hao ndio watayarishaji wa mashindano saba tofauti ya Stevie Awards, ambayo unaweza kujifunza mengi kuyahusu kwenye www.StevieAwards.com. Kombe la Stevie Award limekuwa ndilo mojawapo ya matuzo yanayotamaniwa sana ulimwenguni.
Katika mwaka wa 2024, tuzo la Stevie Awards for Women in Business (Stevie Awards la Wanawake walioko kwenye Biashara) lilipeanwa kwa mashirika na watu binafsi kutoka kwenye zaidi ya nchi 30 katika tukio la tamasha ambalo lilitendeka katika mwezi wa Novemba katika jiji la New York, Marekani. . Bofya hapa ili uone orodha ya washindi wa tukio la 2024.
Kuna aina nyingi za vikundi vya tuzo kwenye tuzo la Stevie Awards for Women in Business (Stevie Awards la Wanawake walioko kwenye Biashara) ambavyo unaweza kuchagua kuwepo. M/Ukiamua kushiriki, utachagua vikundi vinavyolingana na mafanikio ambayo shirika lenu lingependa kutambuliwa kwa ajili yao, na mtayarishe mapendekezo yenu kulingana na maagizo ya vikundi hivyo. Ndivyo hivi aina za vikundi vilivyopo:
- Vikundi vya Tuzo vya Wanawake Binafsi, vikiwemo
- Mwanamke Mjasiriamali wa Mwaka
- Mwanamke Mvumbuzi wa Mwaka
- Mwanamke Mkurugenzi wa Mwaka
- Mwanamke Mwajiriwa wa Mwaka
- Vikundi vya Tuzo vya Kampuni/Shirika (Yanayomilikiwa na Wanawake au Kuongozwa na Wanawake)
- Vikundi vya Tuzo vya Bidhaa & Huduma Mpya (Zilizoundwa kwa ajili ya Wanawake/na Wanawake)
- Vikundi vya Tuzo vya Mawasiliano & Utafutaji Soko (Zilizoundwa kwa ajili ya Wanawake/na Wanawake)
- Vikundi vya Tuzo vya Vyombo vya Habari (Zilizoundwa kwa ajili ya Wanawake/na Wanawake)
- Vikundi vya Mafanikio
Orodha na maelezo kuhusu vikundi hivi yako kwenye furushi/fomu ya kuingilia
Tumeunda orodha yenye sababu kumi zinazoeleza kwa nini shirika lako linapaswa kuwasilisha mapendekezo (watakaozingatiwa kwa tuzo). Pitia orodha hiyo hapa.
Shirika lolote ulimwenguni linaweza kushiriki. Tuzo la 2025 la Stevie Awards for Women in Business (Stevie Awards la Wanawake walioko kwenye Biashara) litatambua mafanikio ya mashirika na watu binafsi kuanzia tarehe 1 Julai 2023.
Kuna makataa tatu au tarehe tatu za mwisho za kujiandikisha au kuwasilisha. Tarehe 25 Juni ndiyo tarehe ya mwisho au makataa ya mapema kabisa, na inatoza ada za kuingilia zilizopunguzwa. Tarehe ya 23 Julai ndiyo makataa ya mwisho au tarehe ya mwisho kabisa. Wanaoingia kama wamechelewa watakubaliwa hadi tarehe 20 Agosti huku wakihitajika kulipa ada ya kuchelewa.
Upendekezaji mtu katika vikundi vingi huhitaji kwamba mtu alipe ada ya kuingililia, lakini kuna baadhi ya vikundi ambavyo unaweza kuingia bila malipo. Ada zozote za kuingilia zinazohitajika zimeandikwa kwenye furushi/fomu ya kuingililia. Lazima ulipe kwa dola za Marekani, labda kupitia kadi ya matumizi/mkopo, hundi au cheki ya benki ya Marekani au kutuma pesa kutoka kwenye akaunti moja hadi nyingine.
Wanafainali wa Tuzo la 2025 la Stevie Awards for Women in Business (Stevie Awards la Wanawake walioko kwenye Biashara) watatangazwa tarehe 19 Septemba. Baada ya hapo, washindi wa Dhahabu, Fedha na Shaba wa Tuzo la Stevie Award watatajwa kwenye tamasha katika Hoteli ya Marriott Marquis jijini New York. Katika tamasha hiyo washindi watapatiwa makombe ya Dhahabu na Medali za Fedha na Shaba za Tuzo la Stevie Award.
Tuzo la Stevie Awards for Women in Business (Stevie Awards la Wanawake walioko kwenye Biashara) lina wawakilishi katika nchi nyingi. Wawakilishi hawa watasambaza habari na kuyasaidia mashirika yaliyoko katika nchi husika kushiriki katika tuzo hili. Ili kujua ikiwa kuna mwakilishi yeyote katika nchi yako,bofya hapa.
Pia, unaweza kuwasiliana na watayarishaji kwa kutumia anwani hii:
The Stevie Awards
10560 Main Street, Suite 519
Fairfax, Virginia 22030, USA
Simu: +1 703-547-8389
Faksi: +1 703-991-2397
Barua pepe: help@stevieawards.com